Dida, Alisema elimu inapaswa kuwa bure kwa Wakenya
wote, na siyo kwa kutegemea mfumo wa ruzuku. Ana digrii ya elimu kutoka
chuo kikuu cha Kenyatta na kwa sasa anafanya shahada ya uzamili katika
masomo ya dini kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi.
Dida amefundisha katika shule kadhaa, ikiwa ni pamoja na
kufundisha fasihi ya Kiingereza na dini katika Shule ya Sekondari ya
Daadab katika kambi mchanganyiko ya wakimbizi na baadaye katika Shule ya
Lenana.
Martha Wangari Karua
Mgombea pekee mwanamke, Martha Karua katika kinyang’anyiro cha urais, alizaliwa Septemba 1957 huko Kirinyaga, Jimbo la Kati.
Karua, mbunge wa Gichugu, anagombea kupitia
National Rainbow Coalition pamoja na aliyekuwa mjumbe wa Baraza la Bunge
la Afrika Mashariki Augustine Lotodo.
Karua ameapa kuwakilisha Muungano wa Kenya pamoja
na jukwaa la mabadiliko ya uchumi na jamii, ikiwa ni pamoja na huduma za
afya kila mahali na kuifanya Kenya kuwa kitovu cha uchumi katika kanda.
Alisema atatoa asilimia 10 ya bajeti ya Kenya
kuboresha uzalishaji wa kilimo, kuongeza vyanzo vya nishati rejezi na
kufanya kazi kuwa ili kuwezesha upatikananji wa intaneti kwa asilimia 50
kwa Wakenya katika miaka mitano. Karua ana shahada ya sheria kutoka
Chuo Kikuu cha Nairobi na shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha
Kimataifa cha Marekani, Nairobi.
Kuanzia mwaka 1981 hadi 1987, Karua alifanya kazi
mahakamani, alipanda kutoka hakimu wa wilaya hadi hakimu mkuu mkazi.
Baada ya hapo amekuwa na shirika la uwakili binafsi hadi 2002. Mwaka
1992, Karua alichaguliwa kuwa mbunge wa Gichugu, kiti ambacho
anakishikilia hadi sasa.
Peter Kenneth
Peter Kenneth
alizaliwa Novemba 1965 huko Bahati, Nairobi. Yeye ni mbunge mwenye
taaluma ya masuala ya benki. Anagombea urais chini ya chama cha Kenya
National Congress, pamoja na mgombea mwenza Ronald Osumba.
Kenneth Pia alidhamiria kuipa polisi vifaa na
kuwalipa vizuri maofisa ili kuwahamasisha kufanya kazi nzuri, na
anaamini kwamba maendeleo na elimu katika maeneo yanayokumbwa na uhalifu
yatazuia vitendo haramu. Anapanga kulipia programu zake kwa kupunguza
matumizi makubwa ya Serikali.
Kenneth ana shahada ya kwanza na ya uzamili katika
sheria kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi, pamoja na kozi ya shahada ya juu
kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Programu ya Utendaji kwa ajili ya
Maendeleo ya Usimamizi huko Lausanne, Uswizi.
0 Comments