Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini na nyota wa Olimpiki,Oscar Pistorius, amefikishwa mahakamani akikabiliwa kwa madai ya kumuua mchumba wake baada ya kupigwa risasi akiwa nyumbani kwa Pistorius mjini Pretoria.
Pistorius aliangua kilio baada ya viongozi wa mashtaka kusema kuwa wataambia mahakama mauaji ya mchumba wake yaliyotokea nyumbani kwake yalikuwa yamepangwa.

Nyumba ya mwanariadha huyo iliyo katika eneo la kifahari mjini Pretoria
baada ya kufikishwa maghakamani , wakala wa Oscar alikanusha madai hayo vikali.
Ombi la dhamana ya mkimbiaji huyo limeakhirishwa hadi Jumanne wiki ijayo,na kwamba yuko mbaroni sasa.
mwaka jana Pistorius alikuwa mwanaruiadha wa kwanza mlemavu kuruhusiwa kushindana na wanariadha wengine wasio na ulemavu kwenye micheco ya Olimpiki, kwam kutumia miguu bandia.
amekuwa na uhusiano na mchumba wake marehemu, Reeva Steenkamp tangu Novemba mwaka jana,na walijulikana na wapenzi wenye kusifika sana nchini humo.

Wataalamu wa uchunguzi, wanatarajiwa kuendelea na uchunguzi wao katika nyumba ya Pistorius ambako mchumba wake Steenkamp, aliuawa.
Duru zinasema kukamatwa kwa Pistorous kumewashangaza wengi sana Afrika Kusini ambako anatazamiwa kama shujaa.
Pistorius alikuwa mkimbiaji wa kwanza mlemavu kuruhusiwa na shirika la kimataifa la riadha kuweza kushindana na wanaridha wengine wasio na ulemavu wowote.
Awali duru zilisema kuwa Pistorius huenda alimuua Reeva Steenkamp kimakosa kwa kudhania kuwa ni mwizi aliyekuwa amemvamia, ingawa polisi walipuuza madai hayo.
Polisi walisema kuwa kumekuwa na visa kadhaa vilivyoriptiwa kutokea nyumbani kwa Pistorius na kutajwa kuwa ugomvi wa kinyumbani.
Pistorius anasifika kama mwanaridha wa kwanza mlemavu kushiriki michezo ya Olimpiki. Habari za mauaji ya mpenzi wake Pistorius zimewashangaza wengi Afrika Kusini kwani anasifika kama mwanaridha anayeiletea nchi hiyo sifa.
Afrika Kusini ni moja ya nchi zenye visa vingi vya uhalifu duniani na watu wengi wanamiliki silaha za kujilinda.