Baba Mtakatifu ameelezea kwamba matatizo ya kiafya yamemfanya kutangaza kujiuzulu.Huko Ujerumani, msemaji wa serikali amesema kuwa anaheshimu kazi kubwa
iliyofanywa na Papa huyu aliyezaliwa katika Jimbo la Bavaria la nchini
humo.Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron, amemsifu Papa kwa jitihada zake za kuimarisha mahusiano baina ya Vatican na Uingereza.
Askofu
mkuu wa Canterbury amesema amazipokea taarifa za kujiuzulu kwa Papa kwa
huzuni mkubwa ingawa anaelewa undani wa hatua yake.
Kiongozi wa Ujeremani, Bi. Angela Merkel amesifu mchango wa Papa wa kupendekeza mjadala baina ya makanisa, waislamu na wayahudi.
Alikumbusha hotuba ya Papa alipozuru bunge la Ujerumani mnamo mwaka 2011.
Uwamuzi na hatua ya Papa Benedict XVI wa
kujiuzulu mwishoni mwa mwezi huu baada ya takriban miaka minane
akiongoza Kanisa Katoliki kwa hoja kuwa umri wake wa miaka 85 ni mkubwa
kiasi kwamba hawezi kuendelea kuhudumu zaidi ya umri huo.
Makao makuu ya Kanisa Katoliki huko Vatican
yanasema yanatarajia Papa mpya atachaguliwa kabla ya mwisho wa mwezi wa
tatu, na sherehe za Pasaka.
Tabia ya kujiuzulu kwa Papa si ngeni, ingawa ni tukio jipya katika karne za hivi karibuni.
Mwandishi wa BBC mjini Roma Alan Johnston
anasema habari hizi zimetokea kama radi, na kwamba hakukua natetesi
yoyote juu ya uwezekano kama huu.
Msemaji wa Vatikani Father Federico Lombardi,
amesema kuwa hata wasaidizi wa Papa wa karibu mno hawakuwa na fununu juu
ya tukio hili.
Kakake Papa huyu mzaliwa wa Ujerumani alipewa
ushauri na Daktari wake asifanye ziara nyingine yoyote ya Marekani na
kwamba kwa miezi kadhaa Mtakatifu Papa amekuwa akitafakari kujiuzulu.
Akizungumza kutoka nyumbani kwake huko Regensburg, Ujerumani, Georg
Ratzinger amesema kuwa Kaka yake alikuwa ameanza kupata shida ya
kutembea na kwamba kujiuzulu kwake ni hatua ya kimaumbile.
Wakati wa kutawazwa kama Papa, Kadinali Joseph
Ratzinger alikuwa mmojawapo wa mapapa wapya kuchaliwa akiwa mwenye umri
mkubwa wa miaka 78.
Alitangazwa Papa mnamo mwezi Aprili 2005 kufuatia kifo cha marehemu John Paul wa pili.
Uongozi wake ulitokea wakati wa wimbi kali la
ubakaji kulikumba kanisa katoliki katika kipindi cha miongo mingi,
ubakaji uliofanywa na watawa dhidi ya watoto wavulana.
Katika taarifa yake, Mtakatifu Papa amesema:
"baada ya kujichunguza binafsi na nafsi yangu mbele ya Mola wangu,
nimefikia uwamuzi kua uwezo wangu na afya, ukiambatana na umri mkubwa,
ni mambo yatakayokwaza jitihada zangu za kuendelea kuliongoza Kanisa
Katoliki.
Kuna kipengele katika sheria ya Kanisa
kinachosema kuwa kujiuzulu kwa Papa kunakubalika iwapo kitendo hicho
kimefanywa kwa hiari na kwa utaratibu unaostahiki. |
0 Comments