Chama tawala cha Kiislamu cha Tunisia, Ennahdha, kmeitisha maandamano
leo katika mji mkuu, Tunis, baada ya umati mkubwa kuhudhuria mazishi ya
kiongozi wa upinzani, Chokri Belaid.Katika ukurasa wake wa Facebook, chama cha Ennahdha kimewaomba watu
wakusanyike saa nane za mchana kulitetea bunge halali ya nchi na kupinga
ghasia za kisiasa.
Huu ndio wito wa kwanza wa maandamano kwa wafuasi wa chama tawala tangu Bwana Belaid kuuwawa siku ya Jumaatano.
Waandamanaji katika mazishi yake Ijumaa, waliilaumu Ennahdha kwa mmauaji yake.
Polisi walifyatua moshi wa kutoza machozi wakati baadhi ya waandamanaji walipochoma moto magari wakitaka mapinduzi mapya. |
0 Comments