Rwanda inapakana na DRC na waasi wa M23 kusaidiwa na jeshi la Rwanda kuendesha harakati zao
Waziri mkuu wa zamani nchini Uingereza Tony Blair, ametetea Rwanda kutokana na madai kuwa inajihusisha na vita Mashariki mwa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Akiongea na BBC, Bwana Blair alisema kuwa sababu za mgogoro huo ni ngumu kuelewa na kuwa serikali ya Rwanda haipaswi kulaumiwa.
Pia alisema ni vigumu kubana msaada kwa Rwanda , hatua iliyochukuliwa na nchi nyingi za kigeni.
Umoja wa mataifa unalaumu Rwanda kwa kusaidia waasi wa kundi la M23 ambao wanalaumiwa kwa kutenda uasi mashariki mwa Congo