Dua ilifunguliwa na baba wa mtoto mwenye kanzu na koti jeusi kwa Fatiha na kuendelezwa na shekh Yusuf na wengine waliofika katika dua ya mtoto Nuhrat.
 Mashekh wetu wa kijiji chetu wakivuta uladi taratibu huku dua zikiendelea..
Huyu ndiye muhusika mkuu wa shughuli nzima ya leo...ni Bidada NUHRAT EDDY mtoto mpya kabisa katika kijiji chetu.Allah amfanyie wepesi katika makuzi yake insh'Allah.
Shekh wetu Yusuf akiendeleza dua mahsusi kwa ajili ya binti mpya NUHRAT katika kijiji chetu hivi leo.
Mzaa chema na huyu ndiye mama Denzel,mama Maysaira na ni mama Nuhrat ukipenda muite Mrs Eddy au jina maarufu kabisa ni Fatma Mashauzi Classic...Maganga One team inakupongeza sana kwa kutuletea mwanakijiji mpya na insh'Allah Allah awafanyie wepesi katika malezi yenu wewe na mumeo.
Huyu ni Mr Eddy ambaye ndiye baba wa mtoto Nuhrat,Ukipenda unaweza kumuita baba Denzel au baba Maysaira,hautakosea ukimuita mume wa Fatma Mashauzi Classic.Ni mwanakijiji mwenzetu hapa Mol.
Kila la heri kwa binti Nuhrat Ameeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeen ...!!!!!
 Dua ikiendelea
 Ally Samba Nahimana naye alishiriki kwenye dua ya binti mpya Nuhrat
 Kina mama na watoto wakipata sadaka ya chakula baada ya dua...
Wazee wa kazi wakiwajibika kama kawaida,yani hapo mtoto hatumwi dukani...
Hii ni familia ya Dullah...Mrs Abby akiwa na watoto wake kwenye kisomo cha Nuhrat leo hii...
 Mazungumzo ya hapa na pale yalikuwepo baada ya dua...
Kutoka kushoto ni Mama Farida,Fatma Mashauzi Classic au Mama Denzel,mama Sharon na mwenye ushungi wwa manjano ni mama Nabil,hapa wakibadilishana mawazo baada ya kisomo cha mtoto Nuhrat.
 Kama kawaida mzee mzima ndani ya nyumba
kama kawaida dada langu la ukweli ndani ya nyumba...kila kitu kilikwenda sawasawa...huyu ni Mrs Yusuph.