Na Musa Mateja KWA mara ya kwanza tangu atoke
mahabusu ya Gereza la Segerea, Dar kwa dhamana, staa wa filamu na video
za wasanii wa Bongo Fleva, Elizabeth Michael ‘Lulu’ au Lizy amefunguka
juu ya uhusiano wake na aliyekuwa mwandani wake, marehemu Steven Kanumba
na kusababisha gumzo kubwa mitandaoni.Huku akipiga picha za pozi kwa mara ya kwanza tangu atoke selo, Lulu
alifunguka wikiendi iliyopita kupitia ukurasa wake katika mitandao ya
Instagram na Twitter kuwa Kanumba alikuwa zaidi ya baba, kaka, mpenzi,
mume, ndugu na rafiki hivyo hataacha kumlilia maisha yake yote. Huku akitanguliza picha ya marehemu Kanumba enzi za uhai wake akipokea moja ya tuzo zake, Lulu aliandika: “Ulikuwa
zaidi ya baba, kaka, mpenzi, mume, ndugu na rafiki…sitaacha kukulilia
katika maisha yangu yote!! R.I.P daddy yangu Steven Kanumba.”Ndani ya muda mfupi, kauli hiyo ya Lulu ilipata maoni mengi huku baadhi
ya watu wakimpa pole kumtia moyo na wengine wakijibizana kwa hasira juu
ya ishu hiyo. Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia marehemu Kanumba ambayo inatarajiwa kuanza kuunguruma muda wowote. |
1 Comments
Public nuisance...Nafsi inakusuta sasa eeh?
Mara una miaka 16, mara umeua bila kukusudia...You will never find peace for the rest of your life...