Stori: Chande Abdallah
KOMEDIAN mkongwe Bongo, Mzee Majuto ameamua kuwachukua wasanii waliotamba kwenye gemu la Bongo Fleva, John Walker na Ras Lion na kuwafundisha komedi.Akipiga stori na paparazi wetu, Majuto alisema lengo lake ni kuona anawaandaa wasanii wengi zaidi kwenye gemu hilo ili aweze kujivunia atakapostaafu kuchekesha.
“Nimefanya nao bonge la komedi, mbali na mimi na kina John Walker, kuna msanii anaitwa Mwala kutoka Kenya naye ameonesha uwezo mkubwa, mashabiki wataiona filamu hiyo hivi karibuni,” alisema Majuto.