Stori: Sifael Paul
ZIkiwa zimebaki siku 8 tu kabla ya hukumu ya staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja kusomwa Machi 25, mwaka huu, inasemekana kuwa baadhi ya mastaa wa filamu na muziki Bongo, wameandaa mkesha wa kumuombea ili hukumu hiyo iende vizuri na aachiwe  huru arudi uraiani, Risasi Jumamosi limetonywa.Kajala anakabiliwa na kesi ya kutakatisha fedha haramu kwa kuuza nyumba iliyokuwa imewekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwa kushirikiana na mumewe, Faraji Agustino.
Kwa mujibu wa mwigizaji mmoja maarufu wa kiume, tayari ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) na ujumbe kupitia mitandao ya kijamii umeanza kusambazwa kwa baadhi ya mastaa hao ambao kila mmoja anaonesha kuwa tayari kwa ishu hiyo ya kumuomba Mungu amsaidie Kajala.