Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dr Hussein Mwinyi.
----------------
SERIKALI
imejiwekea lengo la kutahiri wanaume milioni 2.8 ifikapo mwaka 2015,
baada ya kufanikiwa kuwatahiri 287,055 kati ya mwaka 2010 na 2012.
Hayo
yamebainishwa katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii, ikifafanua kuwa huduma ya tohara ya kitabibu kwa wanaume
ilianzishwa mwaka 2010.
Imetekelezwa zaidi mikoa ambayo ilibainika kuwa na kiwango cha juu cha maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
“Iligundulika
kiwango cha juu cha maambukizi ya VVU ambako kuna kiwango cha chini cha
tohara kwa wanaume. Mikoa hiyo ni ya Iringa, Njombe, Simiyu, Geita,
Katavi, Mbeya, Rukwa, Tabora, Kagera, Mwanza na Mara,” inaelezwa
taarifa hiyo.
Inaelezwa
kuwa Serikali ilifanikiwa kuwafanyia tohara wanaume hao kwa kutumia
njia ya kuwaelimisha kwa kuwaelezea umuhimu wa tohara na hatari
inayowakabili kwa kuendelea kuishi bila kufanyiwa tohara hasa
kuambukizwa magonjwa ya zinaa ikiwamo VVU.
Pia,
taarifa hiyo inaeleza kuhusu mpango wa kuzuia maambukizi ya VVU kutoka
kwa mama kwenda kwa mtoto kwa mwaka 2005, wajawazito 11,435 ambayo ni
asilimia tisa ya wenye maambukizi ya virusi.
Inasema walipatiwa dawa za ARVs kuzuia maambukizi hayo kwenda kwa mtoto.
Taarifa
hiyo inaeleza kuwa, wizara hiyo inaendelea kutoa kupaumbele maeneo ya
kudhibiti magonjwa ya ngono, utoaji ushauri nasaha na huduma kwa
wagonjwa wa nyumbani, elimu na habari, tiba na matunzo, huduma ya
maabara kwa wagonjwa waishio na VVU.
“Hamasa
kwa Watanzania imekuwa ikiongezeka hasa baada ya kampeni iliyoongozwa
na Rais (Jakaya Kikwete) mwaka 2007, idadi ya vituo vya upimaji
iliongezeka kutoka vituo 521 mwaka 2005 hadi 2,200 mwaka jana,” inasema
taarifa hiyo na kuongeza:
“Iidadi
ya wananchi waliopatiwa huduma hiyo nayo imeongezeka kutoka watu
365,189 mwaka 2005 hadi watu 17,008,475 Machi mwaka jana.” ( R &
Ed)
|
0 Comments