Afrika Kusini imetangaza kuwa itatuma wanajeshi Jamhuri ya Demokrasi ya Congo
kujumuika katika kikosi maalumu cha Umoja wa Mataifa cha kuingilia kati nchini
humo ili kuwanyan'ganya silaha wapiganaji.
Taarifa hiyo imetolewa majuma machache tu baada ya wanajeshi 13 wa Afrika
Kusini kuuwawa Jamhuri ya Afrika ya Kati katika hali ya kutatanisha.
Upande wa upinzani umelaani mpango huo, wanasema kuwa haukufikishwa mbele ya
bunge.
Waziri kivuli wa Ulinzi wa chama cha Democratic Alliance, David Maynier,
alisema kuna hatari ya wanajeshi zaidi kupoteza maisha yao.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilitoa idhini mwisho wa mwezi uliopita
kutuma kikosi kitachoweza kupigana na kuingilia kati katika Congo.
1 Comments