Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ametoa mipira zaidi ya 1,200 yenye
thamani ya dola 30,000 za Marekani kwa vyama vya mpira wa miguu vya
mikoa ya Tanzania Bara na vituo 21 vilivyo hai vya kuendeleza vijana
(academies).
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA) lilimpa Rais Tenga fedha hizo ikiwa ni shukrani kwake kwa
kushughulikia mgogoro wa uongozi wa mpira wa miguu nchini Kenya uliodumu
kwa miaka miwili; ambapo nchi hiyo kutokana na mgogoro huo ilikuwa na
vyama viwili (KFF na FKL).
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi
mipira hiyo kwenye ofisi za TFF, Dar es Salaam leo (Aprili 22 mwaka
huu), Rais Tenga amesema amefanya hivyo kwa vile anaamini kuwa mipira
ndiyo kitu muhimu katika kuinua mchezo huo mahali popote.
0 Comments