Alipoondoka madarakani aliwaachia warithi wake, siyo tu wa chama chake cha Conservative bali pia Leba ingawaje msimamo wake ngangari na mara kwa mara wa ubishi ulibainisha utawala wake wa kipindi cha miaka 11 kama Waziri mkuu.
Kwa mda wote wa uongozi ulishuhudia wapiga kura wengi wa kawaida wakifaidi vilivyo, mfano wa kuweza kununua nyumba za manispaa na vilevile kununua hisa katika biashara kabambe ambazo wakati huo ziligeuzwa kua za umma, kama British gas na shirika la simu za mawasiliano BT.
Lakini msimamo wake wa kupinga siasa za mashauriano ulimfanya aonekane kua mtu anayegawanya na hili likasababisha sera zake na mfumo wa uongozi wake kupinga na hatimaye kupelekea wanachama wa chama chake waanze kumpinga moja kwa moja na ghasia kuzuka mitaani.
Ushawishi wa baba
Margaret Hilda Thatcher alizaliwa tarehe 13 October 1925 huko Grantham, Lincolnshire, babake Alfred Roberts, muuza duka la rejareja na mamake, Beatrice.
Babake akiwa mhubiri wa kimethodisti na diwani wa eneo ambaye alimshawishi mno binti yake Margaret na hata kurithi sera zake.
Aliwahi kunukuliwa akisema "kweli, bila shaka namshukuru sana babangu kwa yote. Kweli alinilea na kunifanya niamini yote ninayoyatenda."
Margaret Thatcher alisomea masomo ya sayansi kutoka chuo cha Somerville College, Oxford, na kutokea kua mwanamke wa tatu kua RAIS wa shirika la wanafunzi wafuasi wa chama cha conservative.
Baada ya kuhitimu alihamia huko Colchester alikofanya kazi katika kiwanda kinachotengeneza plastiki na wakati huo huo akishiriki harakati za chama cha Conservative.
Mnamo mwaka 1949, alipendekezwa kama mgombea wa kiti cha mwakilishi wa chama chake cha huko Dartford wilaya ya Kent na licha ya juhudi kali alishindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1950 na 1951.
Hata hivyo aliweza kuweka pengo kwa kupunguza idadi ya wafuasi wa chama cha Leba kama mgombea mdogo kwa umri kutoka chama cha conservative aliyevutia mno vyombo vya habari.
Katika mwaka 1951 alifunga ndoa na mfanya biashara Denis Thatcher, na baada ya hapo kuanza somo la sheria. Alifuzu kama mwanasheria mwaka 1953, mwaka ambamo mapacha wake Mark na Carol walizaliwa.
Alijitahidi bila mafanikio achaguliwe kama mgombea mnamo mwaka 1955 na hatimaye akafanikiwa kujiunga katika bunge kupitia kiti cha conservative cha Finchley wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 1959.
Miaka miwili baadaye aliteuliwa kama waziri mdogo na kufuatia kushindwa kwa chama cha Conservative mnamo mwaka 1964 alipandishwa na kua Waziri kivuli.
'mwizi wa maziwa'
Kiongozi wa wakati huo wa chama Sir Alec Douglas-Home alipojiuzulu, Bi Thatcher akampigia kura Ted Heath katika kinyanganyiro cha mwaka 1965 cha kiongozi mpya na kuzawadiwa wadhifa wa msemaji wa masuala ya makaazi na ardhi.
Alipigia debe haki ya wapangaji wa nyumba za umma kuruhusiwa kuzinunua nyumba hizo na alikua msumari uliokosoa vikali sera za Leba za kodi ya kupindukia.
Ted Heath aliposhinda madaraka na kua Waziri Mkuu mnamo mwaka 1970 aliteuliwa kuiwa Waziri wa elimu kwa maelezo ya kupunguza matumizi ya wizara hio.
Mojapo ya hatua zilizotokana na hilo ni kuondoa mpango wa maziwa ya bure kwa wanafunzi walio kati ya umri wa miaka saba na kumi na mmoja. Hili lilizusha hujuma za chama cha Leba na vyombo vya habari vilivyombandika jina "Margaret Thatcher, milk snatcher" yaani mwizi wa maziwa.
Yeye binafsi alijaribu kupinga uwamuzi wa serikali wa kuondoa maziwa ya bure kama alivyoandika baadaye, nilijifunza somo muhimu. Nilifaidi shutuma kali za kisiasa bila faida yoyote kisiasa."
Akiwa mmoja wa kina mama wachache katika siasa za Uingereza, kulikuwa na fununu kuwa huenda siku moja akawa Waziri mkuu. Tetesi kama hizo zilimzunguka pia aliyekua Waziri katika chama tawala cha Leba Bi.Shirley Williams.
Lakini kama wanasiasa wengine Bi. Thather alipuuzilia mbali madai hayo.
Katika mahojiano ya Televisheni Bi. Thather alisema haamini uwezekano wa kuwepo kwa Waziri Mkuu mwanamke katika maisha yake.
Kutokana na matatizo mengi, Serikali ya Heath haikudumu kwa muda mrefu.
Kutokana na kukumbwa na mgogoro wa mafuta wa mwaka 1973, uliopelekea kupunguza siku za kazi kua tatu kwa wiki nzima halikadhalika mgomo wa wachimba mgodi, serikali ya Thatcher ilizidiwa na mnamo mwezi febuari mwaka 1974 iliachia madaraka.
Thatcher akapewa wadhifa wa Waziri kivuli wa mazingira, lakini alikasirishwa na kile alichokiona kama sera za kigeugeu chini ya Bw.Edward Heath, akaamua kumpinga kwa kuwania uongozi wa chama cha Conservative mnamo mwaka 1975.
Alipokwenda afisini kwa Heath kumfahamisha uwamuzi wake, hakuhangaika hata kumtizama usoni. Alijibu kwa kejeli, utashindwa tu. Na kwaheri.
Kwa mshangao wa wengi, alimshinda Heath katika kura ya kwanza akimsababisha kujiuzulu na kumshinda Willie Whitelaw katika hatua ya pili na hivyo kujitokeza kua mwanamke wa kwanza kabisa kuongoza Chama cha siasa nchini Uingereza.
Moja kwa moja akaonyesha ujasiri wake. Hotuba yake ya mwaka 1976 iliyoshutumu sera za unyanyasaji za utawala wa Sovieti, ulisababisha gazeti moja la huko kumbadika jina la Iron Lady. Kwa kielelezo, Mwanamke mwenye msimamo wa chuma.Binafsi alifurahia jina hilo la utani.
Akitumia msimamo wa mama na mwanasiasa aliyefahamu machungu yaliyosababishwa na mdororo wa uchumi alivihujumu vyama vya wafanyakazi ambavyo hatua yao ya migomo ilisababisha hali mbaya wakati wa majira baridi mnamo mwaka 79.
Wakati serikali ya Bw. Callaghan ilipoanza kuyumbayumba, chama cha Conservertive kilichapisha vipeperushi vyenye kauli mbiu "Labour Isn't Working" yaani chama cha Labour kimeshindwa.
Jim Callaghan alishindwa katika kura ya maoni tareh 28 March 1979. Msimamo madhubuti wa Bi.Thatcher ulikubalika na wananchi wengi na kukipa chama cha Conservative ushindi katika uchaguzi mkuu uliofuata.
Sera ya Fedha
Akiwa Waziri mkuu alijitolea kurekebisha uchumi wa nchi kwa kupunguza mchango wa dola na badala yake kuimarisha soko huria.
Wajibu mkuu wa serkali ulikua ni kupunguza mdororo wa uchumi na punde si punde kuanisha mfumo wa kupunguza matumizi na bajeti.
Sheria zilibuniwa kupunguza malai ya vyama vya wafanyakazi, mashirika ya serikali kubinafsishwa na kuruhusu nyumba za manispaa ziuzwe kwa wananchi wanaoishi humo.
MaMilioni ya watu ambao hapo kabla hawakua na lao wala kumiliki chochote katika uchumi walijikuta wakiwezeshwa kumiliki nyumba zao binafsi na vilevile kununua hisa katika mashirika yaliyokua milki ya dola.
Sera mpya za fedha zikaufanya mji wa London kua mojapo ya miji iliyochangamka na vituo muhimu vya biashara ya kimataifa.
Mifumo ya kale ya viwanda ambayo wakosoaji wengi walilalamika kua imepitwa na wakati na kuweka taka la majengo ya viwanda, yaliondolewa kutoa nafasi katika juhudi za kuunda Uingereza mpya ya kisasa. Ukosefu wa ajira ulipanda kufikia milioni tatu.
Hili lilisababisha mvutano baina ya wanachama waliojulikana kama wets ama wabichi, na hilo pamoja na migomo katika maeneo mengi ya mji yalimzidishia Margaret Thatcher shinikizo za kumtaka arekebeshe sera zake.
Lakini Waziri Mkuu alikataa kutetereshwa. Aliuambia mkutano wa chama wa mwaka 1980: "kwa wale wanaongojea kwa pumzi nzito ya mageuzi kama magazeti yanavyopenda kuandika,nina jawabu moja kwenu. Mnaweza kugeuka mkipenda lakini Mama huyu si kugeuzwa.
Vita vya Falklands
Hadi mwishoni mwa 1981 umaarufu wake ulikua umepungua kufikia asili mia 25%, kiwango cha chini kwa Waziri mkuu yeyote hadi wakati huo lakini juhudi za kufufua uchumi zilikua zimepiga hatua.
Mapema mwaka 1982 Uchumi ulianza kunawiri na kunawiri huko kulimfanya Waziri Mkuu apande miongoni mwa wapiga kura.
Kiwango cha umaarufu wake kilipanda mno mwezi April 1982 kufuatia jibu lake kufuatia uvamuzi wa visiwa vya Falkland kutoka Argentina.
Bila kusita alituma kikosi cha wanamaji na visiwa kukombolewa tareh 14 Juni baada ya vikosi vya Argentina kusalimu amri.
Ushindi huko Falklands pamoja na mtafaruku katika chama cha Leba, kikiongozwa na Michael Foot, yalihakiki ushindi wa kishindo kwa chama cha Conservative katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1983.
Utawala wake ulikumbwa na matatizo mengi, miongoni mwayo mizozo ya
Sera yake Afrika
Margaret Thatcher alimfedhehesha waziwazi Malkia Elizabeth juu ya sera yake juu ya ubaguzi wa rangi wa Makaburu wa Afrika ya kusini. Haya yalibainika alipokabiliana na viongozi wa Jumuia ya madola mwaka 1986 ambapo aliyekua Rais wa ZAMBIA Kenneth Kaunda alitaka Waziri Mkuu wa wakati huo atengwe kutoka mkutano huo wa viongozi.
Bi Thatcher alidai kua vikwazo dhidi ya Afrika ya kusini vingeathiri zaidi mali za Uingereza huko Afrika kusini na masdikini miongoni mwa raia wa nchi ho.
Alikubali Rais wa Afrika ya kusini PW Botha kuzuru Uingereza mnamo mwaka 1984 na kukitaja chama cha ANC kama kundi la kigaidi. Mwaka 1987 alisema kua yeyote anayeamaini kua Chama cha ANC kitaweza kutawala nchi hio kwa kauli yake anaishi katika sayari ya ndoto....Baadaye alikutana na Askofu Desmond Tut ingawa alikataa kukutana na Oliver Tambo. Mwaka 2006 David Cameron akiwa kiongozi wa upinzani aliomba radhi kwa sera yake juu ya Afrika kusini.
Katika mtazamo tafauti na hisia zake kuhusu chama cha ANC na Nelson Mandela, Margaret Thatcher alimsifu mno Robert Mugabe.
Baada ya kuhudhuria karamu aliyomuandalia mnamo mwaka 1982 alimsifu kwa tabia yake ya kirafiki na uwazi. Zimbabwe iliyofanikiwa bila shaka itachangia amani na utulivu katika Afrika ya kati na kusini mwa Afrika kwa ujumla, na tunakutakieni wewe na wenzako katika jitihada zenu, haya yamo katika maandishi yake binfasi.
Ingawa alikorofishana na Kenneth Kaunda mnamo mwaka 1986 uhusiano wao haukuwa wa uhasama. Katika juhudi ya kutafuta suluhu ,bw Kaunda alimualika wacheze densi wakati wa mkutano wa viongozi wa Jumuia ya madola uliofanywa mjini Lusaka mnamo mwaka 1979, Kaunda likumbusha katika mahojiano na BBC baadaye.
Bi Thatcher aliizurui Nigeria mara mbili. Akiwasili mjini Lagos mnamo mwaka 1988 alimvisha sifaa tele kiongozi wa kijeshi wakati huo General Ibrahim Babangida na kuelezea uwiyano uliopo baina ya Mataifa yao mawili. Hata hivyo ziara yake hiyo ililenga fungamano la mikataba ya biashara ya mafuta.
Wakati wa ziara yake hio alitembelea Kenya. Nigeria na Kenya zikionekana kama nchi zinazoipenda Uingereza. Baada ya kuchunguza miradi katika Rift Valley - na kuvishwa mauwa ya Kimasai Bi Thatcher akampaka sifa Rais Moi kwa muongozo wake wa amani na utulivu. Pia aliusifu moyo wa Harambee nchini Kenya akiulinganisha na sera za Uingereza.
Mwaka huo wa 89 alizuru Zimbabwe na Malawi na kutembelea Namibia bila kutarajiwa. Wadadisi wanasema kua ziara yake hio ilikua chachu ya kuanzisha mchakato wa Uhuru wa nchi hio.
Labda la kushangaza kwa nchi iliyokua chini ya utawala wa Kisoshalisti -raia wa Msumbiji walimpenda Iron Lady na kumfananisha na kiongozi wao shupavu Samora Machel.
Mwanawe Margaret Thatcher Mark pia alihusika mno na masuala barani Afrika - ingawa kwa hali ya kuaibisha. Mwaka 1982, alipotelea katika jangwa Sahara kwa mda wa siku sita wakati akishirtiki mashindano ya mbio za magari maarufu kama Dakar Rally.
Mwaka 2005 alikiri kua alivunja sheria zinazokataa mamluki nchini Afrika kusini kwa ununuzi wa ndege iliyotumiwa katika jaribio la kuipindua serikali ya Equatorial Guinea. Alipewa kifungo cha miaka minne nje ya jela.
chanzo cha habari hizi ni BBC Swahili.
0 Comments