Milipuko miwili katika eneo la kukamilisha mbio ndefu za Boston imesababisha majeruhi wasiojulikana idadi yao.

Picha na video kutoka Boston zinaonyesha watu wakiwa wamechanganyikiwa wasijue pa kwenda, huku magari ya huduma za dharura yakielekea katika eneo la tukio na watu waliojeruhiwa vibaya wakipelekwa kwenye hema la matibabu ya haraka.

"Kuna watu wengi wamelala chini," alsiema mwanariadha mmoja akinukuliwa na chombo cha habari cha AP.

Tukio hilo linaripotiwa kutokea saa tatu baada ya washindi kuvuka mstari wa ushincdi.

"Kulikuwa na mlipuko, polsi, moto na EMS kwenye eneo latukio. Hatuna namna ya kutulekeza namna watu walivyojeruhiwa," msemaji wa Polisi Boston alisema.

AP linasema kulikuwa na sauti kubwa ya mlipuko upande wa kaskazini mwa mtaa wa Boylston Street, karibu tu daraja linaashiria mstari wa kumalizia mashindano. Mlipuko mwingine ukasikika dakika chache baadaye.

Mike Mitchell wa Vancouver kutoka Canada, mwanariadha aliyemaliza kukimbia alisema alikuwa akiangalia nyuma ya mstari wa kumalizia mashindano ndipo aliposikia ‘mlipuko mkubwa’

Inataarifiwa kuwa moshi ulipanda juu hewani kiasi cha futi 50 (mita 15),' aliliambia shirika la habari la Reuters , na watu wakaanza kukimbia wakipiga mayowe baada ya kusikia

"Kila mtu alichanganyikiwa,’ alisema.

Waliokuwa wakimalizia mbio hizo waliongozwa kuepuka eneo lenye moshi kwenye mlipuko wakati huo huo eneo hilo likifungwa.

Tawi la Msalaba Mwekundu la Mashariki mwa Massachusetts limetenga kituo cha kusaidia majeruhi.