Jesli la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu sita ambao wanajihusisha na vitendo vya kishirikina kwa kujifanya wanaagua na kufichua watu wachawi katika vijiji mbalimbali. Wanaenda mbali zaidi na kudai wanafichua watu wachawi wanaozuia mvua isinyeshe katika maeneo mbalimbali hapa Dodoma. Watuhumiwa hao hujulikana hapa Dodoma kwa jina maarufu LAMBALAMBA. Watuhumiwa walikamatwa tarehe katika kijiji cha MBALAWALA.[picha na maelezo kwa ihsani ya Michuzi]
Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma David Misime akielezea ukamatwaji huo na kuonesha tunguli walizokuwa wanatumia