SERIKALI YA TANZANIA YASAINI MKATABA WA MABILIONI KUTOKA BENKI YA DUNIA


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yapokea shilingi bilioni 314 kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya kusaidia miradi ya Umeme, Gesi, Bajeti ya Serikali pamoja na kuwajengea uwezo wa kuendesha miradi ya gesi. Mkataba huo umesainiwa leo na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt Wiliam Mgimwa Waziri wa fedha, pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier Mjini Washington DC.

 Waziri wa Fedha Mhe Dkt. Wiliam Mgimwa pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier wakijadiliana jambo kabla ya kusaini mikataba hiyo.

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa wakibadilishana mkataba na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier.