Mwakilishi
wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi,
akifuatilia kwa makini majadiliano ya Mkutano wa pili uliokuwa
ukijadili uandaaji wa malengo mpya ya maendeleo endelevu ( SDGs).
Mkutano
huo ulifanyika kwa siku tatu hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na
ni mmoja wa milolongo ya mikutano ya majadiliano yanayolenga kuunda
malengo hayo endelevu ili kuendeleza maudhui ya malengo ya Milenia
ambayo mipango yake itafikia tamati Mwaka 2015.
Tanzania
ni kati ya nchi Thelathini ambazo zimechaguliwa kuongoza majadiliano
hayo. Akichangia majadiliano hayo, Balozi Tuvako Manongi, pamoja na
mambo mengine alisisitiza kwamba malengo mapya ya maendeleo pamoja na
kuzingatia mihimili mitatu ya ajenda za maendeleo yaani uchumi, jamii
na mazingiria, suala la kuendeleza mapambano dhidi ya umaskini lazima
liwe lengo kuu katika malengo hayo mapya.Nyuma ya Balozi, Ni Afisa
Ubalozi Mwandamizi, Bw. Modest Mero
0 Comments