Mwezeshaji Akifafanua na kutoa uelewa kwa wakinamama washiriki wa mdaharo kuhusu ardhi, hifadhi au maeneo ya pembezoni mwa Mito na kuwataka wanawake watafute ardhi hata kwa kununua.
Wanawake waliohudhulia mdaharo wa wanawake, wakiandika masomo ya mada wanazojifunza ikiwa ni kwa siku ya tatu.
Kutoka Kushoto, Jane Kapongo, Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliyehudhuria kusikia na kujibu changamoto mbalimbali za ardhi zinazowakabili Wanawake.
Mshiriki kutoka kijiji cha Nghaya wilaya ya Magu akielezea mgogoro wa ardhi na kuvunjiwa nyumba kwa wakazi waishio pembezoni mwa mto Simiyu.

Mdahalo wa Kitaifa wa Wanawake Jana uliingia siku ya tatu ambapo mada kuu ilikuwa Haki za Wanawake katika rasilimali za asiliambapo mada ndogo ndogo kama sera ya ardhi na sheria ya ardhi ya kijiji ya Tanzania, umuhimu wa wanawake kumiliki ardhi na rasilimali nyingine pamoja na uwekezaji wa ardhi na madhara yake kwa wanawake zilijadiliwa.
Mada ndogo nyingine zilikuwa ni pamoja na nafasi ya wanawake katika jamii yenye rasilimali pamoja na wanawake wazalishaji chakula, upatikanaji na umiliki wao wa rasilimali muhimu..

Jopo la wataalamu wa maswala ya ardhi lilikuwepo kusikiliza na kujibu maswali mbalimbali yaliyojitokeza. Wataalamu hao walikuwa ni Bernard Baha (Mwanaharakati wa maswala ya Ardhi), Victoria Mandari ( Mwanasheria wa kujitegemea), Yifred Miyenzi (Mkurugenzi Haki Ardhi), Juvenile Rwegasira (Mwanasheria kutoka TAWLA, Lilian Loloitai (Afisa kutoka CORDS) pamoja na Enock Kijo (Mwanaharakati wa maswala ya Ardhi)

Vilevile Jane Kapongo, Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi alikuwepo kusikiliza na kujibu baadhi ya changamoto zilizotajwa na wanawake hao.

Mdahalo wa Kitaifa wa wanawake ni tukio linalofanyika kwa hisani ya mtandao wa jinsia wa asasi za kiraia (CSO Gender Coalition) kuanzia tarehe 10-14 April, 2013 mkoani Dodoma.

Mdahalo huu umewaleta pamoja wanawake wapatao 300 walioko pembezoni (marginalised) kutoka katika mikoa yote ya Tanzania.

Tunachukua fursa hii kuwasihi wananchi wote wafuatilie kwa makini mdahalo huu kupitia mitandao ya kijamii na tovuti rasmi iliyozinduliwa na Mhe. Sophia Simba (MB), Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.


Twitter: www.twitter.com/SautiYaMwanamke  #MdahaloWaWanawake

Facebook: www.facebook.com/SautiYaMwanamke

Tovuti: www.sautiyamwanamke.org