Taarifa za karibuni kabisa zinaeleza kuwa mtu mmoja amekufa kwenye mripuko
uliotokea katika ufunguzi wa kanisa la Katoliki la Olasiti, kwenye kitongoje cha
Arusha, Tanzania.Watu kama 50 wamejeruhiwa.
Makamo wa rais wa Tanzania, Dr. Mohamed Gharib Bilal amewasili Arusha kwenda
kupeleka pole ya serikali kwa viongozi wa kanisa na majeruhi.
Dr. Bilal alisema serikali ya Tanzania itafanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa
inawapata watu waliohusika na mripuko huo.
Mtu mmoja amekamatwa lakini haikuelezwa ni nani au kama amehusika na kundi
lolote. |
0 Comments