Leo ni siku ya mama duniani..sina maneno yenye utamu juu ya mama ila neno MAMA halina mfano na lina uzito kwa wale wenye kujua thamani ya mama.Nawatakia mama wote duniani siku njema yenye fanaka kwao na iwe siku yenye furaha na kuendeleza upendo kwa watoto wao.Maganga One Blog inashirikiana na mama wote duniani kusheherekea siku hii kwa mapumziko na wazazi nyumbani,hivyo siku ya leo sitakuwa na news kwa watu wangu mnaokuwa bega kwa bega na Maganga One Blog.

Nawatakia jumapili nzuri na tuwe karibu na wazazi wetu kadri itakavyowezekana,asanteni sana.
MAGANGA ONE.