'Waathiriwa watafurahi'
Tume hiyo ilipewa jukumu la kuchunguza na kupendekeza hatua zinazofaa
kuchukuliwa kuhusu ukiukwaji wa haki za binaadamu katika kipindi kati ya uhuru
wa Kenya Desemba mwaka 1963 na mwisho wa Februari 2008 --mkiwemo ghasia
zilizochochewa kisiasa,mauaji,ufisadi na migogoro ya ardhi.
Bw Farah alisema ripoti hiyo imekua tayari kukabidhiwa kwa Rais tangu
Alhamisi Mei 2-lakini tume hiyo haikuweza kupata miadi ikulu kwa sababu ya
shughuli nyingi za Bw.Kenyatta.
"nimeambiwa na mwanasheria mkuu kwamba iwapo tu ripoti yetu iwe na muhuri wa
tarehe 2 Mei ,basi inaweza kukabidhiwa hata wiki ijayo.," Bw Farah ameiambia
BBC.
Alisema hakuweza kufichua maelezo kuhusu mapendekezo hayo hadi pale
itakapochapishwa rasmi.
Lakini uwezo wa tume hiyo umemaanisha lazima kuwe na aina fulani ya haki "ili
kuwaridhisha waathiriwa", alisema.
"tumependekeza baadhi ya watu wafunguliwe mashtaka lakini ikumbukwe
tueshughulikia pia maswala ya maridhiano-kuganga makovu; umoja na mambo kama
hayo ."
Bw Farah, ambae amesema mapendekezo ya tume hiyo ni jukumu la lazima ni mmoja
wa Wakenya watano katika tume hiyo;wajumbe wengine watatu wanatoka Ethiopia,
Marekani na Zambia.
Makataa ya kuwasilisha ripoti hiyo kwa Rais yamekwishaongezwa muda wake kwa
kipindi cha miezi sita.
Raila Odinga, aliyekua waziri mkuu katika serikali iliyopita ya kugawana
madaraka na aliyeshindwa uchaguzi wa Rais mwezi Machi alikiri kuwa mchakato huo
umecheleweshwa mara kadhaa. Ripoti hiyo ilikua ikabidhiwe kwa aliyekua Rais Mwai
Kibaki.
"lakini tulihisi ingetifua mambo ambayo yangeleta athari katika uchaguzi.
Aliambi kipindi cha Newsday cha BBC. '
Odinga ambae aliekwa kizuizini kwa muda wa miezi sita wakati wa utawala wa
aliyekua Rais Daniel arap Moi, alisema yeye hana wasiwasi wowote na ripoti hiyo
kwa sababu hana kitu cha kuficha.
Rais Uhuru Kenyatta atafanya ziara ya kiserikali mjini London wiki ijayo,
"ikiwa kuna chochote dhidi yangu niko tayari kuwasikiliza " alisema .
"watu hawatazamii kutakua na taaifa za kushtusha,watu wanatarajia ukweli.
Kama ujuavyo baadhi ya nyakati ukweli unauma lakini Biblia inasema ukweli
utatukomboa " Alisema Bw Odinga .
"hebu tuwache kufichaficha dhulma hizi ambazo zimechangia kuwepo kwa chuki
miongoni mwetu"alisema
"tunataka mambo haya yagfichuliwe ili jamii yetu iweze kuridhiana na kusonga
mbele kama taifa moja lilioungana."
Akiongea kuhusu kushindwa kwake katika uchaguzi , Mr Odinga alisema imempasa
akabiliane na hali yha kuvunjika moyo kwa kushindwa. .
"mimi mwanamichezo na najua michezo kama hii ina maokeo ya aina mbili tu. Ni
kama mzigo mzigo umetuliwa sasa nahisi nimepumua"
Bwana Kenyatta anatarajiwa kuwasili Uingereza wiki ijayo kwa mwaliko wa
serikali ya Uingereza kuhudhuria mkutano kuhusu mustakbala wa Somalia. . |
0 Comments