Na Hamida HassanKWELI haya ni makubwa! Baada ya kuadimika kwa muda mrefu, mwigizaji wa filamu za Kibongo, Aisha Bui ameibuka na kusema kuwa anatafuta mwanaume ambaye atamzalia mtoto na hatimaye waoane ila akadai wa kumuoa kwa sasa hamuoni.

Mwigizaji wa filamu za Kibongo, Aisha Bui.Akizungumza na chanzo cha habari hizi,  Aisha alifunguka kuwa alikuwa kimya kwa sababu kuna mambo alikuwa akifanya.
Alisema kwa kuwa ameyakamilisha, sasa ana nafasi ya kusaka mtoto iwapo atampata mwanaume sahihi.
Alivitaja vigezo vya mwanaume wa kumzalia kuwa amjengee nyumba ya kuishi yeye na mtoto wake kisha awe na uwezo wa kumlea na kumpatia elimu bora.