Ofisi za Gaeti la Daily Monitor zilizovamiwa na polisi wa Uganda
Polisi nchini Ugandan wamevamia ofisi za magazeti kufuatia
taarifa kwamba Rais Yeweri Museveni anamuandaa mwanawe wa kiume kumrithi
urais.
Vituo viwili vya Redio pia vamiwa na kuzimwa , hii ni kwa muujibu wa gazeti
la serikali la New Vision.
Wiki iliyopita magazeti ya Uganda yalidai kuwa kuna njama za kuwaua wale
watakao pinga mpango wa Rais Museveni kumuandaa mwanawe kuchukua madaraka ya
Uganda.
Magazeti hayo yalidai kuwa mipango hiyo ya mauaji yalitolewa na Mkuu fulani
wa jeshi la Uganda.
Bwana Museveni, ambaye amekuwa madarakani tangu 1986, anatarajiwa kung'atuka
uongozini mwaka 2016.
Kwa muda mrefu kumekuwa na madai kwamba Museveni anamuandaa mwanawe Muhoozi
Kainerugaba,ambaye ni brigadier jeshini kushikilia uongozi wa Uganda.
Lakini serikali ya Museveni imekanusha kwamba kuna mipango kama hiyo.
Mwanawe Museveni Brig. Kainerugaba.
Wiki iliyopita gazeti la, the Daily Monitor,na jengine la , Red Pepper,
lilichapisha barua ya siri ikidai ilikuwa imeandikwa na Jeneral David Sejusa,
ikitaka uchunguzi ufanywe kuthibitisha madai kwamba kuna mipango ya kuwauwa wote
watakao piga mipango ya Rais Museveni kumpachika mwanawe uongozini.
Uvamizi huo wa polisi umeidhinishwa na mahakama ya Uganda na ulikuwa unalengo
la kutafuta barua hiyo inayodaiwa kuandikwa na mkuu huyo wa Jeshi akifichua
njama za mauaji.
Vituo viwili vya Redio vinavyohusiana na Daily Monitor, Dembe FM na KFM, pia
vilivamiwa na kuzimwa. |
1 Comments