Wapiganaji wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)  wamewasili mji wa Goma, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kujiunga na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani.
Wiki iliyopita, Amiri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete alikabidhi Bendera  kwa Kiongozi wa Bataliani ya wapiganaji wa JWTZ wanaokwenda nchini humo, kwenye hafla iliyofanyika Msangani Kibaha, Mkoa wa Pwani.
Machi mwaka huu, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lilipitisha mpango wa kupeleka wanajeshi  Mashariki mwa Congo, lengo likiwa ni kulinda amani kwa kushirikiana na majeshi ya Serikali kuwaondoa waasi wa M23  walioko Mashariki mwa nchi hiyo.