Mh.Ali Siwa,mwakilishi wa Ubalozi wa Tanzania,Berlin akitoa hotuba ya Ufunguzi

Mh.Ali Siwa wa Ubalozi wa TZ Berlin,akizungumza na Mzee.Katabalo (mtumishi mstaafu wa UN).

Dada Nashe Mvungi akionyesha bidhaa za Tanzania kwa wageni.

Wageni wakijichagulia Bidhaa za Tanzania
Maana ya muungano yakubalika na watoto wa kimataifa !ngoma inogile.

Dada Tabia Mwanjelwa(mwenye) gitaa akiwa na wasanii wenzie jukwaani

Wageni mbali mbali wakiipongeza Tanzania, mwenyekiti wa UTU Mh. Mfundo aliyevaa shati la kitenge akiongoza shughuli.

Watanzaia wautingisha Mji wa Koloni Ujerumani!
 
Chereko ! Chereko za Sherehe za miaka 49 ya muungano wa Tanzania !
Siku ya Jumamosi 27.04.2013 Watanzania Wanaoishi Ujerumani , chini ya mwamvuli wa umoja wao (UTU) Waliuhakikishia ulimwengu kuwa neno "MUUNGANO" lina maana
kamili kwa maisha ya  mtanzania na binadamu wengine.
 
Sherehe hizo zilizowakusanya watanzania na marafiki wa Tazania kutoka kila kona  ya ujerumani, ziliutingisha mji wa koloni katika Usiku usio kwisha wa kusherehekea miaka 49 ya muungano wa Tanzania.
 
Mhe.Ali Siwa naibu balozi wa Tanzania nchini Ujerumani alikua mstari wa mbele akiwaongoza watanzania katika Muungano Day,
Wasanii mbali mbali walitumbuiza jukwaani na kuipeperusha vilivyo bendera ya Tazania.
Mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania ujerumani Mh.Mfundo na kamati yake wameahidi
kufanya mambo makubwa na kuitangaza  Tanzania kwa hali na mali chini  ya  Umoja wa watanzania Ujerumani(UTU)