Wakuu wa Iraq wanasema wamegundua njama ya al-Qaeda kutaka kutumia silaha za
kemikali nchini Iraq na kuzisafirisha kwa magendo hadi Ulaya na Marekani.Msemaji wa wizara ya ulinzi, Mohammad al-Askari, alisema idara ya usalama ya
jeshi imegundua karakana tatu za kutengeneza kemikali hizo, pamoja na kemikali
ya kuharibu neva.
Bwana al-Askari aliiambia televisheni ya Iraq kwamba wanaume watano
walikamatwa baada ya kuchunguzwa kwa miezi mitatu.
Wote walikiri makosa, alisema. |
0 Comments