Mahsein Awadh ’Dk. Cheni’ akiwa na jembe lake.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo la kusikitisha lilijiri maeneo ya Viwanja vya Leaders Kinondoni, Dar hivi karibuni wakati staa huyo akitaka kuondoka eneo hilo. Habari zilitonya kuwa vijana hao wakiwa na pikipiki (bodaboda) walimfuata Dk. Cheni na kuanza kummwagia vitisho wakimhoji kwa nini amekuwa ‘klozi’ sana na Lulu. Bila kufafanua ukaribu wa mastaa hao wa filamu unawakera nini, wavamizi hao walipasua vioo vya gari la Dk. Cheni aina ya Mitsubishi Pajero.
ILIKUWAJE HASA? Shuhuda wetu alisimulia kuwa wakati wa tukio hilo Dk. Cheni na Lulu hawakuwa pamoja, jambo lililomfanya msanii huyo kupigwa na butwaa asijue la kuwajibu wale vijana na kuacha hatma yake mikononi mwa watekaji.
BAADA YA KUPASUA KIOO “Walipopasua kioo cha mbele cha gari upande wa dereva, vijana wale waliondoka na kumwacha Dk. Cheni akiwa hajui cha kufanya,” shuhuda alisema. Hata hivyo, inadaiwa wakati vijana hao wakimtaiti Dk.Cheni walisikika wakitaja jina la Kanumba bila kufafanua anahusika vipi na kitendo chao cha kumvamia msanii huyo. Inaelezwa kuwa jitihada za msanii huyo kuwadhibiti wahalifu wale wa amani hazikuweza kuzaa matunda na hivyo kumfanya nguli huyo wa filamu kuhesabu hasara ya kioo hicho.
DK CHENI ALIRIPOTI POLISI? Amani lilipomuuliza ‘sosi’ huyo kama Dk. Cheni alikwenda kuripoti polisi, jibu la swali hilo lilikuwa ni hapana, sababu ikiwa ni mtendwa kushindwa kukariri namba za pikipiki. “Alishauriwa aende polisi lakini akasema hawezi kufanya hivyo kwa sababu wahusika hawafahamu na kwamba hana ushahidi wowote wa kuwafanya watuhumiwa wakamatwe
HUYU HAPA DK. CHENI Baada ya kupata taarifa hizo, Amani lilimsaka Dk. Cheni ambaye alikiri kuvamiwa na watu hao na kupasua kioo cha gari lake lakini hawakumjeruhi. “Kumekuwa na matukio mengi ya ajabuajabu yananitokea, nadhani hivi sasa nitakuwa makini sana, nitaripoti polisi kila kitu, siwezi kuendelea kupuuzia,” Dk Cheni alisema.
TUJIKUMBUSHE Dk. Cheni alijitahidi kwa hali na mali kumsaidia Lulu kutoka gerezani Segerea akikabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia katika kifo cha Kanumba aliyefariki dunia Aprili 7, mwaka jana ambapo alisota kwa muda wa takribani miezi kumi hadi alipotolewa kwa dhamana ya shilingi milioni 20, mwezi Machi mwaka huu. Hivi karibuni Dk. Cheni alilazwa katika Hospitali ya Buruhani iliyopo maeneo ya Posta, Dar, baada ya kula chakula kilichosadikiwa kuwa na sumu. Matukio hayo yanazidi kuibua maswali mengi na akitakiwa kuwa makini zaidi.
|
0 Comments