Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na
Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokea tuzo ya Millenium Development
Goals, Women Progress Awards 2013, kutoka kwa Ms Jennie Yeung , Rais wa Shirika
la Sun Zhong Shan Foundation lililo chini ya United Nations Education, Science,
Cultural and Health Advancement  Foundation la nchini Marekani.  Mama Salma alipokea tuzo hiyo baada ya
kutimiza baadhi ya malengo ya Millenia katika masuala ya ukimwi, elimu kwa watoto
waliokosa fursa  na kuwawezesha wanawake
kiuchumi nchini Tanzania. Kulia ni Katibu wa WAMA, Ndugu Daud Nassib na kushoto
ni Dr. Judy Kuriansky, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Columbia nchini Marekani.

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete
akimkabidhi tuzo hiyo Katibu wa WAMA Foundation , Ndugu Daud Nassib  wakati wa kupokea   tuzo
hiyo huko New York nchini Marekani tarehe 13.6.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipongezwa na Dr. Judy Kuriansky, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Columbia mara tu baada ya kukabidhiwa tuzo yake.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia
waalikwa waliohudhuria sherehe za utoaji tuzo kwa wake wa Marais wa Bara
la afrika zilizofanyika huko New York nchini Marekani. Picha na John Lukuwi