Jumamosi hii ya tarehe 8/6/2013 ndani ya ukumbi wa Gemeente ya Mol nchini Belgium kutafanyika sherehe za ufunguzi wa Chama cha Umoja wa Waafrika wanaoishi Mol na vitongoji vyake.Katika sherehe hizo kutaambatana na burudani mbalimbali zikiwemo ngoma za asili toka Burundi,muziki wa mwambao wa pwani toka Visiwa vya Zanzibar na muziki wa Hip hop n` Rnb kutoka kwa msanii wa Holland.
|
Msanii Walid toka Holland pia atakuwepo |
Milango itakuwa wazi kuanzia saa tisa na nusu mchana,vyakula aina mbalimbali vya kiafrika vitakuwepo.Burudani zitaanza mapema mpaka saa nne usiku.
Msanii Ally Khamis ambaye ataimba siku hiyo ya jumamosi tarehe 8/6/2013.
Mataifa yote mnakaribishwa na jinsi ya kufika anuani ni kama ifuatavyo.
Molenhoekstraat 2
2400 Mol
Kwa mawasiliano zaidi unaweza kutuandikia kwa njia ya email-
magangaone@gmail.com
0 Comments