Mamia ya watu wanaendelea kukusanyika nje ya hospitali
alikolazwa Nelson Mandela mjini Pretoria Afrika Kusini. Inaarifiwa Mandela bado
yuko hali mahututi.
Wamekuwa wakimuimbia nyimbo na kumuombea nje ya hospitali. Wengine
wamekusanyika katika iliyokuwa makaazi ya Mandela mtaani Soweto.
Watu wana wasiwasi kuhusu hali y mandela lakini pia wanataka kuonyesha
wanavyojivunia kiongozi wao ambaye wanamuona kama baba wa taifa lao.
Mandela , rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini, anaugua maradhi ya Mapafu.
Mamia ya wananchi walikesha kwa maombi maombi nje ya makaazi ya zamani ya
aliyekuwa rais wa taifa hilo Nelson mtaani Soweto.
Rais Jacob Zuma amesema kuwa afya ya shujaa huyo aliyepigana dhidi ya ubaguzi
wa rangi nchini humo inaendelea kuimarika.
Mandela aliye na umri wa miaka 94 amekuwa hospitalini akiuguwa ugonjwa wa
maambukizi ya mapafu.
Awali mwanawe wa kike, Makaziwe alisema afya ya babake inaendelea kuwa
njema.
Aidha Makaziwe amevikashifu vyombo vya habari kwa kukita kambi nje ya
hospitali alikolazwa shujaa huyo akisema wanahabari wanapaswa kumheshimu
babaake.
Rais Jacob Zuma alisema Alhamisi kuwa hali ya Mandela iliimarika lakini bado
yuko hali mahututi.
"leo angalau yuko sawa kidogo kuliko nilivyomwacha jana usiku,'' alisema Rais
Zuma baada ya kuongea na madakatari wanaomtibu Mandela.
Bwana Zuma alifutilia mbali safari yake ya Msumbiji ili kumtembelea Mandela
hospitalini.
Wakati huohuo mwanawe Mandela Makaziwe alisema Mzee 'bado yupo' na kuwa
anaweza kuhisi mtu akimgusa. |
0 Comments