Picha kutoka maktaba
MKOA wa Kagera,unakabiliwa na wimbi la wahamiaji haramu wanaokadiriwa kufikia 32,000 ambao huingia njia za panya. Naibu Kamishina wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kagera George Kombe aliiambia MTANZANIA mjini Bukoba jana.

Alisema wahamiaji hao, wanaingia mkoani hapa kupitia maeneo ya Murongo, Kanyigo, Rusumo, Mtukura, Bugango na Kabanga.

Alisema kutokana na kuwepo kwa wahamiaji hao, idara yake inakadiria kutumia Sh milioni 650, kwa ajili ya kufanya operesheni ya kuwarudisha makwao.

Alisema wahamiaji wengi, wanatoka nchi za Rwanda, Burundi, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC).


Alisema pamoja na idadi hiyo, bado wanaendelea na kazi ya kuwatambua wahamiaji wengine.

Alisema, pamoja na jitihada hizo, bado kuna baadhi ya viongozi wakiwamo wenyeviti wa vitongoji ambao wanawahifadhi majumbani mwao.

Alisema mwaka 2006, walifanya operesheni kama hiyo ambapo walitumia Sh milionin 450.