Stori:Johannesburg,Afrika Kusini
Mashirika makubwa ya habari ulimwenguni, yapo kwenye vita nzito ya kugombea hakimiliki ya mazishi ya Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Rolinhlala Mandela ‘Madiba’.Shirika la Habari la Afrika Kusini (SABC), kwa sasa lipo kwenye mzozo na lile la Uingereza (BBC), mvutano uliopo unahusu chombo chenye haki ya kuwa cha kwanza kutangaza taarifa zote zitakazohusu mazishi ya Mzee Madiba.
Awali, SABC ndicho chombo kilichotajwa kama cha kwanza kupewa hakimiliki ya matangazo yote ya mazishi ya Madiba lakini taarifa mpya ni kwamba mjukuu wa Mandela, Mandla Mandela, 37, anadaiwa kuvutiwa na dau la BBC, hivyo kuliuzia haki zote shirika hilo la Uingereza.
Inadaiwa kuwa BBC limempa Mandla, randi 3,000,000 (zaidi ya shilingi milioni 615), hivyo kulinyima haki SABC ambalo awali lilikuwa limetoa randi 2,000,000 (zaidi ya shilingi milioni 326).
Upande mwingine, vyombo vya habari vya kama CNN, Sky, Al-Jazeera na vinginevyo, kila kimoja kinasaka hakimiliki hiyo, huku baadhi vikiwa vimefunga mitambo ya kurusha moja kwa moja (live), matangazo na taarifa za maendeleo ya Madiba kutoka kwenye Hospitali ya Mediclinic Heart, alikolazwa.
Kitendo cha vyombo hivyo kufunga mitambo hiyo kwenye hospitali aliyolazwa Madiba, kinatafsiriwa kama mwendelezo wa mchuano, ikidaiwa kwamba si kwamba lengo lao ni kurusha maendeleo ya afya ya mzee huyo, bali kupata mapema taarifa za kifo kwa haraka na kutangaza.
HAYO YANAFANYIKA MZEE AKIWA MAHUTUTI

Tafsiri rahisi ni kwamba huo ni uchuro, kwani mvutano huo unatokea katika kipindi ambacho Madiba hali yake ni mahututi.
Madiba, amelazwa hospitalini hapo akisumbuliwa na tatizo mapafu, maradhi ambayo yanatajwa kwamba ni athari ya kifungo cha miaka 27 jela alichofungwa mwaka 1963, kipindi ambacho alikuwa anaongoza vita dhidi ya sera za ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.


MANDELA ADAIWA KULAZIMISHWA KUKANUSHAMandla, amekanusha kuuza hakimiliki kwa BBC lakini tovuti ya shirika la habari la Telegraph, Afrika Kusini, iliandika kwamba alilazimishwa kukanusha.
Iliandika kuwa kila kitu kipo wazi kwamba Mandla aliuza hakimiliki za matangazo ya mazishi ya Madiba kwa BBC.
Mandla alisema: “Sina makubaliano ya kimaandishi si kwa SABC wala BBC, vilevile kwa chombo kingine chochote kwa ajili ya hakimiliki ya kutangaza mazishi ya Nelson Mandela. Hakuna makubaliano yoyote.”

MKE WA MANDLA ATOBOA
Mke wa kwanza wa Mandla, Thando Mabunu-Mandela, amekiri kwamba mume wake aliingia makubaliano na SABC tangu mwaka 2009.
Thando alisema, anajua kila kitu kuhusu makubaliano hayo, kwa hiyo ni vema Mandla akaweka kila kitu kisheria na kuutangazia umma.
Hata hivyo, Thando na Mandla kwa sasa wameshatengana lakini mwanamke huyo amedai kwamba kipindi makubaliano yanafanyika, walikuwa bado ni mke na mume.
“Mandla ndiye kiongozi wa ukoo kwa sasa, kwa hiyo anatakiwa atoe tamko la kisheria kuhusu hili suala, maana mimi najua kila kitu kuhusu makubaliano ya kifedha na SABC kwa ajili ya mazishi ya Madiba,” alisema Thando.

TUZIDI KUMWOMBEA MANDELAKwa namna yoyote ile, Madiba ni nembo ya Bara la Afrika, tuzidi kumwombea ili kwa kudura za Mungu, aweze kunyanyuka tena. Tunaamini mbele ya Mungu hakuna kinachoshindikana. Amina.
                                                                      
                                                                   Chanzo cha habari gonga hapa.