BISMILLAH RAHMANI RAHIM
 
Assalam aleykum ndugu waislam wote kila kona ya dunia.Napenda kuitumia nafsi hii kuwatakia heri na wepesi ndani ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
 
Kwa kuwa huo ndio mwezi mahsusi wa kutubia dhambi zako,ewe ndugu muislam tumia nafasi hii kujiepushaa na yale yote yatakayomkasilisha Allah s.w. na badala yake hakikisha kila jambo unalofanya linampendeza Allah s.w. ili uwe miongoni mwa watakaofaulu siku ya malipo.
 
Fitna,kusengenya,chuki na kila baya kwa mwenzio hakikisha unajisafisha kiukweli ili upate dhawabu na malipo mema ndani ya mfungo huu mtukufu wa Ramadhani.kusema uongo ama utani ambao hauna faida ndani ya mfungo wa Ramadhani ni vyema ukajiepusha navyo hivi vitu.
 
Nakuusia wewe ndugu yangu muislam na kuiusia nafsi yangu pia..huu sio mwezi wa mchezo hata kidogo ni mwezi wa kuchumaa hasa,hivyo tuitumie nafasi hii kwa kufanya yaliyo mema kwa Allah s.w.
 
Suala la kufanya Ibada ni muhimu sana kwani lina faida nyingi .Hii ni katika kukumbushana Allah ni mjuzi zaidi yangu.
Nawatakia kila jepesi na heri ndani yangu waislam wote duniani.Ramadhani Karim.
Wabillah taufiq.
 
Maganga One - Blogger.