Wataalamu hao wamesema zaidi ya asilimia 80 ya fedha zinazotolewa katika benki kuu nchini humo zinatumika kwa mambo binafsi huku matumizi ya asilimia 33 ya mapato ya kila mwezi ikiwa ni mapato ya shughuli za bandari hayajulikani yanatumika vipi na asilimia 4 pekee ya mapato ya nchi yanayotokana na shughuli za kutoa hati za usafiri ndio yanayoifikia serikali ya Somalia.
Katika ripoti iliotolewa kwa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wataalamu hao wanaoangalia kwa makini vikwazo dhidi ya Somalia wamesema jambo linalozua hali hii ni kuwepo kwa gavana wa sasa wa benki kuu ambapo dola milioni 12 kati ya dola milioni 16.9 ziliowekwa katika benki hiyo na shirika la PricewaterhouseCoopers hazijulikani ziliko.
0 Comments