Spika wa Bunge la Jamhuri ya Korea Kusini wikiiliyopita alihitimisha  ziara ya sikutatu hapa nchini aliyoianza tarehe 8 hadi 10 Julai 2013 ambapo alikutana naviongozi wakuu wa Taifa. Awali alikutana na Rais wa Jamhuri yaMuungano waTanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne S.Makinda. Spika huyo pia akiambatana na Naibu Spika wa Bunge laTanzania Mhe.Job Ndugai aliizuru Zanzibar na kukutana na  Rais wa Serikaliya Mapinduzi Zanzibar Dkt.Mohammed Shein na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. A.P. Kificho. 
 Wajumbe wa mkutano kwa upande wa Tanzania


 Picha ya pamoja ya viongozi hao baada ya mkutano ambao baadhi ya mambo yaliyozungumziwa ni pamoja na Korea kuuwekeza hapa nchini
katika Nyanja ya TEHAMA.

Spika Makinda akimkabidhi mgeni wake zawadi marabaada ya chakula cha jioni.
Spika Kang akipokelewa na Spika wa Baraza la
Wawakilishi Mhe. A.P. Kificho mara tu baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege
wa Zanzibar

Rais wa Zanzibar Dkt. Mohammed Shein (kulia)
akiwa na mazungumzo na Spika wa Bunge la Korea Kusini Mhe. Kang Chang-Hee (kushoto).
Katikati ni mkalimani

Picha ya pamoja kwenye Ikulu ya Zanzibar.

Rais wa Zanzibar Dkt. Mohammed Shein
akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Job Ndugai (Mb) wakati wa ziara ya Spika wa Korea visiwani Zanzibar.


Spika wa Bunge la Korea Kusini Mhe. Kang
Chang-Hee akiushukuru ujumbe wa Tanzania kwa heshima kubwa mara baada ya
kumaliza ziara yake hapa nchini. (Na Prosper Minja - Bunge).