Tanzania inapendekeza kufanyiwa, marekebisho sheria ya kulinda
amani, kuwezesha vikosi vya kulinda amani kujikinga na mashambulizi.
Hii ni baada ya walinda amani saba wa Tanzania kuuawa na watu waliokuwa
wamejihami eneo la Darfur mwishoni wa wiki.
Wanajeshi wengi walijeruhiwa baadhi wako mahututi.
Mauaji ya walinda amani 7 wa Tanzania nchini Sudan imewashangaza wengi sana
nchini humo kulingana na naibu waziri mkuu kwani nchi hiyo ndio imeanza kushika
kasi katika juhudi zake za amani kimataifa. .
Maafisa hawakuwa na taarifa kamili kuhusu uvamizi wa Jumamosi ambapo
wanajeshiu wengine 17 walijeruhiwa vibaya katika shambulizi baya zaidi
kushuhudiwa dhidi ya vikosi vya kimataiofa nchini Sudan.
Shambulizi hilo lililofanywa na kikundi kikubwa cha watu waliokuwa
wamejihami, ilihusisha mashambulizi makali ya mizinga na iliyolenga wanajeshi
hao umbali wa kilomita 25 Magharibi mwa mji wa Khor Abeche.
Tanzania, ambayo pakubwa ni nchi salama na thabiti katika Kanda ya Afrika
Mashariki, imeendelea kujitolea sana katika juhudi za amani duniani.
Mwaka jana ilikuwa nchi ya kwanza kujitolea kupeleka vikosi vyake Mashariki
mwa Congo, chini ya kile ambacho kitakuwa kikosi cha walinda amani wa Umoja wa
Mataifa wenye jukumu la kupambana vilivyo na makundi ya waasi huko. |
0 Comments