Umoja wa Watanzania Ujerumani (U.T.U ) Kushiriki katika Festival ya
"Brüderschaft der völker " mjini      Aschaffenburg " Ujerumani.
                   Kuanzia leo Ijumaa 19 hadi 21 Julai 2013

Watayarishaji wa Festival ya "Brüderschaft der völker " mjini Aschaffenburg,
nchini Ujeruamani,wameuhalika Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) kushiriki katika maonyesho hayo utamaduni wa nchi mbali mbali yatakayoananza  Leo ijumaa 19 hadi  jumapili 21 Julai 2013.anza  Leo ijumaa 19 hadi  jumapili 21 Julai 2013.
Watayarishaji wa maonyesho hayo wamevutiwa sana sana na shughuli
za Umoja wa Watanzania ujerumani (UTU) kwa juhudi zake za kuitangaza
Tanzania,wandaaji wa onyesho hilo wametoa nafasi kwa umoja wa watanzania kushiriki na kuitangaza Tanzania kwa kasi zaidi.
Mwenyekiti wa UTU Bw.Mfundo Peter Mfundo ameupokea mwaliko
huo kwa mikono miwili na amewaomba Watanzania wote wanaoishi
ujerumani kujitokeza kwa wingi katika maonyesho hayo na kuitumia
nafasi waliyopewa kwa maslahi ya Tanzania na watanzania, Umoja wa
Watanzania (UTU) utakuwa na banda lake katika maonyesho hayo.
Mnakaribishwa wote na kwa maelezo zaidi wasiliana na
Mhe.Mfundo,mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania Ujerumani(UTU)