Umoja wa mataifa hii leo umeanza kupeleka wanajeshi wake nchini
Mali na kufikisha idadi ya wanajeshi wanaoshika doria nchini humo na ambao
watakuwa chini ya UN hadi, 6,000.
Idadi ya wanajeshi inatarajiwa kufika 12,640 mwisoni mwa Disemba.
Umoja wa Mataifa utachukua jukumu la kushika doria kutoka kwa jeshi la
Ufaransa ambalo lilisimamia operesheni ya kuwafurusha wapigananji wa kiisilamu
kutoka Kaskazini mwa nchi mwezi Januari.
Jukumu lake la kwanza litakuwa kuhakikisha kuna usalama kabla ya uchaguzi wa
urais kufanyika tarehe 28 mwezi huu.
Wapiganaji wa kiisilamu walianza kufanya harakati zao baada ya mapinduzi ya
kijeshi yaliyomwondoa mamlakani rais wa taifa hilo huku wapiganaji wa kiisilamu
wakitwa udhibiti wa eneo Kaskazini mwa nchi hiyo ikiwemo miji ya Gao, Kidal na
Timbuktu ambako waliamuru kutumika kwa sheria kali za kiisilamu.
Ufaransa iliamua kuingilia mzozo huo, baada ya wapiganaji wa kisilamu
kutishia kuvamia mji mkuu Bamako.
Tangu mwezi Januari, wanajeshi 4,000 wa Mali, wamechukua udhibiti wa sehemu
kubwa ya miji mikubwa nchini humo, lakini wapiganaji kadhaa wamekuwa wakifanya
mashambulizi ya kuvizia,
Jeshi la Umoja wa mataifa litajulikana kama Minusma na litahitaji kufanya
kazi nzuri.
Harakati za jeshi la Ufaransa zimewafurahisha wengi kwa sababu wamekuwa
wakitumia nguvu.
Lakini waasi wametoroka na wananchi wengi wa Mali wanahofia kuwa wanajeshi wa
UN huenda wasitumie nguvu kama wanavyofanya wanajeshi wa Ufaransa. |
0 Comments