Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwaaga wananchi wa Kijiji cha Mkenda, Songea Vijijini baada ya kuweka jiwe la msingi kijijini hapo akiwa katika ziara ya mkoa wa ruvuma Jaulai 19, 2013. Katikati ni Mkewe Tunu na kulia ni Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na askari wa Msumbiji wakati alipopita kwenye mpakakati ya nchi hiyo na Tanzania katika kijiji cha Mkenda akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 19,2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu wakiteta na Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama (kushoto) baada ya kuwasili kwenye kijiji cha Mpitimbi kuzindua msimu wa ununuzi wa mahindi Julai 19, 2013. Walikuwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipima katika mzani gunia la mahindi kuashiria uzinduzi wa msimu wa ununuzi wa mahindi katika kijiji cha Mpitimbi akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 19, 2013. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu. [ picha kwa ihsani ya Michuzi ]
0 Comments