Watu wakipata misosi kando ya barabara bila hata ya wasiwasi wa magonjwa.
WAUZA vyakula kama vile ndizi-choma, mishikaki, soseji na kadhalika wamekuwa wakifanya hivyo kwa muda mrefu katika Mtaa wa Lindi karibu na Shule ya Uhuru, Kariakoo kwenye kituo cha mabasi ya kwenda Mbagala.  Vyakula hivyo huuzwa katika mazingira machafu ambayo ni hatarishikwa afya za watu kwani huwa havifunikiwi dhidi ya mavumbi, inzi na uchafu mwingine.
                              (PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY)