Bundi wa Ras Makunja hawana ukorofi na mtu,
Baada ya kujichukulia tuzo ya kimataifa ya
bendi bora ya kiafrika barani ulaya,mkuu wa kikosi kazi cha Ngoma Africa band aka FFU kamanda
Ras Makunja alikutwa akicheza na bundi wake katika maskani yake "Anunnaki Empire" alipoulizwa 
kulikoni awapende bundi hao ! kwanini asifuge ndege kama kasuku ? Kamanda Ras Makunja alijibu heti "Bundi wake" hawana ukorofi na mtu
ni ndege wenye upendo tuu tena watulivu kuliko Kasuku,Kamanda Ras makunja amedai kasuku wana kelele sana..lakini Bundi wakimya na wapole.
Alipoendelea kuhojiwa akaamua kuuchuna.