Mwenyekiti wa jumuiya ya watanzania jijini New York nchini Marekani ndugu Hajji Khamis Hajji alipomtembelea Maganga One Blogger hapo jana..Pichani kutoka kushoto ni Maganga One,Hajji Khamis Hajji na katibu wa kijiji bwana Mohamed kulia.
 Kipindi cha kiangazi watu wengi tunaoishi barani Ulaya hupendelea kukaa nje mpaka saa nne za usiku kutokana na kuchelewa kwa jua kuzama..pichani BBQ ikichukua nafasi yake hapo jana.

 Tukipata picha ya pamoja na ndugu Hajji kabla hajaaga hapo jana..Bwana Hajji yupo nchini Belgium kwa mapumziko[likizo]kabla hajarudi kuendelea na shughuli zake nchini Marekani.
Mwenyekiti wa New York Tanzanian Community akiagana na Katibu Mohamed hapo jana nyumbani kwa Maganga One alipokuja kututembelea.tunakutakia kila la heri katika safari yako Mwenyekiti Bwana Hajji na tunakukaribishana tena nchini Belgium.