Ashley Toto
Ijumaa ya leo ukurasa wetu unapambwa na msanii wa kutoka Kenya mwenye makazi nchini Germany na huyo si mwengine bali ni msanii mwenye mvuto wa kimahaba kwa jina Ashley Toto.Ni muigizaji mzuri sana kwenye sanaa na sasa anakuja kimataifa zaidi.

Akiongea na Maganga One Blog Ashley alisema ``Nashukuru kwamba mashabiki wangu wananikubali kwa kazi ambazo najaribu kuwaonyesha nikizifanya...kama Mungu akinijaalia soon nitakwenda Africa na kucheza filamu na wasanii wengi wenye majina makubwa kwenye industry hiyo ya filamu...Maganga One Blog ilipojaribu kumuhoji kama alikuwa na majina ya wasanii hao...Ashley Toto alisema`` kwa sasa sio vizuri nikiweka kila kitu wazi ila niwathibitishie watu wangu kwamba ni kweli nitafanya movies na watu wenye majina makubwa Africa``.

Maganga One Blog ilipomuuliza kama alikuwa tayari kutaja baadhi ya nchi ambazo anatarajia kwenda kufanya movies hizo..Ashley alisema `` Kwanza kabisa nitapenda kwenda TANZANIA kwani kiukweli katika ukanda wa Africa Mashariki na kati Tanzania wamepiga hatua kiasi kwenye Tasnia hii ya filamu za kiswahili``.

Mahojiano yalipoendelea  Maganga One Blog ilitaka kujua kiufupi maisha ya Msanii Ashley...
Ashley alifunguka kama ifuatavyo
:Ashley ``Mmmh [kicheko] sijui nianzie wapi?
Maganga One : Anzia kokote tu msanii wetu
Mpenzi msomaji wa Maganga One Blog usikose mahojiano haya kati ya Msanii Ashley Toto na Blog yako ya Maganga One wiki hii..Utapata kujua Ashley ni nani..anataka nini na siri ya Urembo wake ni nini.Stay tuned.