Sherehe za ufunguzi wa sikukuu ya Eid  katika kitongoji cha Harelbeke jijini Kortijk zilifunguliwa kwa ibada maalum...
Kwa upande wa kina mama waliofika katika sherehe hizo hapo jana hawa ni baadhi yao wakiwa na nyuso za furaha ya sikukuu.
Hapa kina mama toka France,Holand na kwengineko nao walifika katika sherehe hizo
Na mabinti kutoka sehemu mbalimbali nao walikuwepo katika sikukuu hizo...
               Baadhi ya mashekh waliofka kwenye sherehe wakibadilishana mawazo
    Wageni waalikwa wakiwa wametulia kusikiliza yanayojiri shughulini hapo
Hapa kila mmoja anatoa chake na kusikilizwa kwa makini na wanachangia maneno kiungwana zaidi
                                              Story na mawaidha yanaendelea
Wakati wa maakuli ulipofika kila mmoja alijumuika kupata chakula....wallah chakula kilikuwa kitamu sana..Allah awajaalie wote walioiandaa shughuli nzima.
Brother Rasheed baada ya mfungo wa Ramadhan sasa ameamua kurudisha uzito kwa kasi..
Baadhi ya wakazi wa Harelbeke wakipata chakula cha sikukuu
 
                       Maganga One  uso kwa uso na Pasua Kichwa....
 Tuliojumuika kwenye sikukuu tukipata picha za kumbukumbu
 Ally Samba akiwa na mama yake toka nchini Ufaransa wakiwa na nyuso za furaha siku ya jana..
                                                         Menu ya nguvu...
         Kila aina ya chakula kitamu kilikuwepo hapo..kazi ilikuwa kwa walaji tu..
                       Mduara wa kupata riziki ukiendelea kuchukua nafasi
 Mashekh walioiongoza vyema shughuli ya sikukuu kwa Quran tukufu na mawaidha hapo jana..Allah awafanyie wepesi insh`Allah
 Mashekh wakipata riziki
 Kila panapokuwa na watoto ujue kuna heri na Baraka...jana watoto waliburudika kwa kujumuika na kucheza pamoja.
Mash`Allah vijana hawa wa kizungu wa wamebahatika kuingia katika dini ya Kiislam na kukubali kuungana na waislamu wenzao kwenye sikukuu hapo jana..pichani wakipata chakula cha pamoja.
                                                 Mr Dietman Maganga One...
 Kina mama wakiwa wametulia vyema kabisa pamoja kwenye sikukuu hapo jana
 Mmoja wa kina mama aliyehudhuria sherehe za sikukuu hapo jana
 Maganga One nikiwa na mwenye nyumba ambapo palifanyika shughuli hiyo..Allah amfanyie wepesi mzee wetu kwa mapokezi mazuri kwa wageni tuliofika kwenye sherehe za la Eid hapo jana..
ukitaka kuona picha nyinginezo yabonyeze maandishi ya blue yaliyoandikwa read more