Ndege ndogo aina ya Vich Grave, yenye namba za usajili 5H /EPW mali ya TanzaAir baada ya kuanguka ziwani. |
.Ikiwa kwenye maji. |
Abiria sita na rubani wamenusurika kufa baada ya ndege ndogo aina ya Vich Grave waliyokuwa wakiruka nayo kupata dharura na kuanguka katika Ziwa Manyara jana.
Imelezwa kuwa ndege hiyo yenye namba za usajili 5H /EPW mali ya TanzaAir ilipata hitilafu katika injini yake moja hatua ambao ilimlazimu rubani wake aliyetambulika kwa jina moja la Kapteni Kondo (51) kuishusha lakini ikaanguka kwenye ziwa hilo.
Abiria hao walipata majeraha madogo madogo na kukimbizwa hadi Hospitali ya Selian inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Kati jijini hapa kwa matibabu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema ndege hiyo ilikuwa ikitokea Bukoba kwenda jijini Dar es Salaam kupitia Zanzibar.
Aliwataja abiria hao kuwa ni Anik Kashasa (51), Regina Mtabihirwa(58), Aloyce Mwanga (60), Naburi Meeda (80), Ashura Mohamed (38)pamoja na Protas Ishengoma (45) wote wakazi wa jijini Dar es Salaam.
Alisema abiria hao waliokolewa kwa kutumia mitumbwi ya wavuvi na kisha walichukuliwa na chopa hadi Arusha kwa matibabu.
0 Comments