Bunge la Uruguay limepitisha mswada wa kuhalalisha bangi. Ikiwa
mswada huu utapitishwa na Baraza la Senate, Uruguay itakuwa nchi ya kwanza
kuhalalisha uzalishaji na utumiaji wa bangi.
Hatua hii inaungwa mkono na serikali ikisema itapunguza mapato na faida kubwa
kwa walanguzi wa mihadarati pamoja na kuwafanya watumizi wa bangi kutotumia dawa
kali za kulevya.Chini ya mswada huo ni serikali pekee itakua na kibali cha kuuza
bangi.
Pia serikali itatoa utaratibu wa uzalishaji, mavuno, uhifadhi na mauazo ya
nje. Wanunuzi wote watanakiliwa kwenye daftari maalum na sharti wawe wametimiza
miaka 18 na zaidi. Mteja anaweza tu kununua kilo 40 kwa mwezi kutoka kwa maduka
ya dawa au kukuza mimea sita ya bangi.Wageni hawatakubaliwa kununua bidhaa
hii.
Wabunge 50 kati ya 96 walipitisha mswada huo. Wanaotetea kuhalalishwa kwa
bangi wamesema vita dhidi ya mihadarati havijapiga hatua na ipo haja kuweka
mbinu mpya.
Kwa miongo mingi kanda ya Latin America imekumbwa na ghasia za magenge ya
mihadarati ambapo maelfu ya watu wamekufa. Matukio ya Uruguay yanatazamwa kwa
karibu eneo hilo ikiwa yatasaidia kupunguza machafuko yanayotishia uthabiti wa
mataifa mengi. |
0 Comments