Siku ya jumamosi tarehe 31 mwezi wa 8 mwaka huu 2013 katika ukumbi wa Theater de Vaillant jijini Den Haag patakuwa hapatoshi...Ni siku ya ufunguzi wa Filamu ya kwanza ya kiswahili kuchezwa nchini Uholanzi.

Njoo uione kwa macho yako movie yote mwanzo mwisho siku hiyo..Ikiwa bado haitoshi washiriki wote waliocheza movie watakuwepo ukumbini kupokea ushauri wenu na maoni.Ili kufanikisha kila mmoja aweze kuja kuiona movie hiyo kiingilio ni sawa na bure euro 5 tu ushindwe wewe hapo.


Ukumbi ni wa kisasa ambao una siti 140 tu hivyo hautapata dhambi ukiwahi tiketi yako mapema mlangoni kabla ya kuchelewa..anuani ni kama ifuatavyo
Theater de Vaillant
Hobbema straat 120

2526kt,den haag
Holland.
Haitaruhusiwa kwa mtu yoyote kusimama ukumbini..ukichelewa tiketi ujue umekosa uhondo wa karne..ukumbi utakuwa wazi kuanzia saa kumi kamili jioni.Movie itaanza saa kumi na nusu..kumbuka mambo yote yatakwenda kwa kujali muda.

MUHIMU.
Haitaruhusiwa mtu yoyote kurekodi movie hiyo iwe kwa simu ya mkononi,Ipad n.k.Tunategemea ushirikiano wenu ili kuungana kama familia moja..Waafrica haijalishi umetoka nchi gani njoo ujionee movie hiyo..kwa wasioelewa kiswahili vyema movie ina SUBTITLE...kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana nasi kwa email magangaone@gmail.com
 simu no +32 466 164 772-Maganga One
 au +31 641 653 067 Hija Salehe