Hapa ndipo ufunguzi wa movie utafanyika....wahi siti yako mapema kwani kila kitu kitakwenda kwa time.

Ile movie iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na watu wengi ndani na nje ya nchi sasa imekamilika..Njoo ushuhudie vijana wapya ambao wamejaribu kukuonyesha uwezo wa juu kisanii katika tasnia hii ya filamu.Haijawahi kutokea na usisubiri kuhadithiwa maana uhondo utauona mwenyewe siku ya jumamosi tarehe
31/08/2013 a ndani ya jiji la waungwana Den Haag nchini Uholanzi .Siku hii ni siku ya Ufunguzi ndio siku itakayoonyeshwa movie nzima ndani ya ukumbi wa T
heater de Vaillant,ukumbi utakuwa wazi kuanzia saa kumi kamili jioni...tiketi zitauzwa hapohapo mlangoni kwa kiasi kidogo sana ambacho kila mmoja atakimudu ni euro 5 tu.Movie itaanza kuonyeshwa saa kumi na nusu hivyo ukichelewa utakosa uhondo wa wasanii wapya ambao wamekuja kivingine kabisa.
Wahi siti yako mapema kwani haitaruhusiwa mtu kusimama akiwa anaangalia Utamu huu wa karne.Ukumbi kama unavyouona hapo juu pichani...
Anuani ni kama ifuatavyo:-

Theater de Vaillant
Hobbema straat 120

2526kt,den haag
Holland.

Angalia kautamu kadogo ka Movie nzima hapa chini..Yani ni balaa