Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya na nchi za Ubelgiji, Luxembourg na Uholanzi  Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiwa katika picha ya pamoja na Wana-Diplomasia wa Serikali ya Uholanzi baada ya chakula cha mchana kilichoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufalme wa Uholanzi  kumuaga rasmi Uholanzi baada ya Serikali ya Tanzania kuamua  kuufungua Ubalozi wa Tanzania Uholanzi uliofungwa mwaka 1994 na kuendelea kusimamiwa na Ubalozi wa Tanzania Ubelgiji. 

Kutoka kushoto ni Bw. Maarten Wammes (Mkuu wa Idara wa Sera za Nje), Bw. Michael Stibbe (Mkurugenzi wa Idara ya Afrika ), Bi. Grace Shangali (Kaimu Mkurugenzi wa Ulaya na Amerika - Tanzania), Bw. Govern Jan Bijlde Vroe (Mkurugenzi wa Itifaki), Mhe. FransHakkerberg (Balozi wa Heshima wa Tanzania Uholanzi) , na Bw. Marten De Boer (Mratibu wa Sera wa Afrika ). Balozi mpya wa Tanzania Uholanzi, Mhe Wilson Masilingi anatarajiwa kufika kituoni hapo wakati wowote.