Katibu wa Jumuiya ya Tanzania akielezea nini maana ya GLN na kwanini Jumuiya ya Tanzania DMV ni moja ya washiririki
Banda la Tanzania lilkiwa limetembelewa na wageni mbalimbali kujionea vitu vilivyoletwa wakiwemo walimu wa darasa la kiswahili DMV kwenye maonyesho ya Global Language Network yaliyofanyika Washington, DC kwa kushirikisha nchi mbalimbali na Tanzania ikiwa ndio mara ya kwanza kushiriki kwenye maonyesho hayo.
Baadhi ya nguo zilikuwepo kwenye banda la Tanzania ndani ya maonyesho ya Global Language Network yaliyafanyika Jumamosi Sept 28, 2013 kwa ushirikiano wa chuo kikuu cha New York (NYU) na Tanzania kushiriki kwa mara ya kwanza na banda lao kuvutia wageni wengi hasa kwenye chakula walicholeta chai na vitafunio mbalimbali.
Wageni wakiwa kwenye foleni ya kupata chai ya Tanzania na vitafunio kama vile Vitumbua, maandazi na kadhalika na wengine wakijionea nguo na vitabu vya kiswahili.
Wageni wakiendeea kujionea, kula na kusikiliza vivutio vingine vilivyopo Tanzania kwa Walimu wa darasa la kiswahili DMV wakijaribu kuwaelezea uzuri wa Tanzania na vivutio vyake.
Walimu wa darasa la kiswahili wakiwaelezea wageni waliotembelea banda la Tanzania upikaji wa vitafunio walivyoleta.
Mmoja ya mgeni aliyetokea Virginia akipata chai na kitumbua huku akisifia utamu wake.
Walimu wa darasa la kiswahili katika picha ya pamoja.
Watoto wa darasa la kiswahili wakiimba baadhi ya nyimbo za Tanzania
Mgeni akipata maelekezo ya vitabu vya kiswahili huku akiwa na kibakuli cha maandazi.
Banda la Tanzania katika picha ya pamoja.
Mzee Safari (kulia) akimuelezea moja na mgeni kuhusu kitabu chake cha "Nyao za Obama" alichatunga kwa Kiswahili
0 Comments